Bobi avunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa mbwa mwenye umri mkubwa zaidi

 


Mbwa wa Ureno mwenye umri wa miaka 30 ametajwa kuwa ndiye mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kutokea duniani na Guinness World Records - akiipiku rekodi iliyodumu kwa karne moja.


Bobi ni aina safi ya Rafeiro do Alentejo - aina ambayo ina wastani wa kuishi miaka 12 hadi 14.


Habari hizi zinakuja wiki mbili tu baada ya Spike the Chihuahua, 23, kupewa rekodi ya mbwa mwenye miaka mingi Zaidi .


Mbwa wa zamani zaidi kuwahi kutokea alikuwa Bluey wa Australia, ambaye alikufa mnamo 1939 akiwa na umri wa miaka 29 na miezi mitano.


Kufikia 1 Februari, Bobi alikuwa na umri wa miaka 30 na siku 226.


Hili limethibitishwa na hifadhidata ya wanyama kipenzi ya serikali ya Ureno, ambayo inasimamiwa na Muungano wa Kitaifa wa Madaktari wa Mifugo, kulingana na Guinness World Records.


Ameishi maisha yake yote na familia ya Costa katika kijiji cha Conqueiros, karibu na pwani ya magharibi ya Ureno, baada ya kuzaliwa na ndugu watatu katika jengo la nje.


Leonel Costa, ambaye alikuwa na umri wa miaka minane wakati huo, alisema wazazi wake walikuwa na wanyama wengi na ilimbidi kuwaweka chini watoto hao, lakini Bobi alitoroka.

Post a Comment

0 Comments