Halmashauri Ya Tarime Mjini Kukabidhiwa Jengo La Ofisi Ifikapo Februali 15 Mwaka 2023

 


Na Timothy Itembe Mara.


MADIWANI wa halmashauri ya mji wa Tarime wameazimia kukabidhiwa jingo la ofisi za halmashauri ifikapo Februali 15 mwaka 2023 ili kulitumia na kuondokana na adha kukodi ukumbi wa mikutano ya Baraza.


Kauli hiyo ilitolewa baada ya Baraza la madiwani kujadili na kupitisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2021,2022-2023 kilichokalia ukumbi mpya ambapo waliomba kukamilishiwa kwa haraka jingo hilo ili kuokoa gharama zinazotumika pindi wanapokuwa na uhitaji wa ukumbi wa mikutano ya Baraza na mahitaji mengine ya kiofisi.


Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Daniel Komote alisema Baraza lake limeazimia kukabidhiwa jingo la ofisi ili kulitumia kwa manufaa ya halmashauri na kuondokana na adha inayowapata pindi wanapokuwa wanauhitaji wa ofisi na mikutano.


Komote alisema endapo hawatakabidhiwa Ofisi hizo kwa mda uliopangwa yeye ataita vyombo vya habari na kutangaza siku maalumu ya kuhamishia Ofisi yake hata kama jengo halitakuwa limekamilika hiyo itakuwa mfano wa kuigwa kama alivyoamuwa Rais Joseph Pombe Magufuli wakati wa uhai wake alioutumia wakati wa kuhamia makao makuu Dodoma.


Mwenyekiti huyo alisema Baraza lake limependekeza mkaguzi wa ndani kufuatilia sintofahamu ya shilingi milioni 101 ndani ya siku 14 ambazo zinadaiwa kutumika kinyume cha utaratibu wa kiasi tengwa shilingi milioni 50 kwenye ujenzi wa kituo cha Aya Chomete ambapo awali Naibu Waziri TAMISEMI aliagiza uchunguzi wa fedha hizo ufanyike kujua matumizi yake halisi.


Naye mkuu wa Divisheni ya mipango na utaratibu,Victor Fredrick akisoma bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2023-2024 alisema mapendekezo ya mpango wa bajeti umezingatia vipaumbele 09 ikiwemo kukamilisha miradi vipolo.


Afisa huyo aliongeza kuwa halmashauri yake kwa mwaka wa fedha 2023-2024 inaomba kuidhinishiwa mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2023-2024 shilingi Bilioni 26.7 kwa matumizi ya vyanzo vya ndani,Mishahara,Ruzuku toka serikali kuu na miradi ya maendeleo.


Katika Baraza hilo Joseph Haymu,Utumishi alisema halmashauri yake imewapandishia kodi wafanyabiashara wa vibanda soko la Rebu kutoka shilingi 15,000-20,000 na kwenda shilingi 50,000 kwa mwezi na vibanda vya stend ya magari kutoka shilingi 40,000 hadi shilingi 100,000 kwa mwezi ili kuongeza makusanyo ya mapato.

Post a Comment

0 Comments