Nyota wa tenisi akiri kumshambulia mpenzi wake wa zamani lakini akakwepa kukutwa na hatia

 


Nyota wa tenisi wa Australia Nick Kyrgios amekiri kumpiga mpenzi wake wa zamani lakini akaepuka kukutwa na hatia ya uhalifu.


Kukiri hatia kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 katika mahakama ya Canberra kulifanyika baada ya mawakili wake kushindwa kufutilia mbali shtaka hilo kwa misingi ya afya ya akili.


Bw Kyrgios alimsukuma Chiara Passari kwenye barabara ya lami wakati wa malumbano huko Canberra mnamo 2021, mahakama ilisikia.


Hakimu aliliita tukio hilo "kitendo kimoja cha kijinga au cha kufadhaisha" wakati wa kumuepusha na rekodi ya uhalifu.


Mambo yaliyokubaliwa yaliyowasilishwa kortini yanasema kwamba Bw Kyrgios alimsukuma Bi Passari baada ya kusimamisha gari lake lisiendeshe walipokuwa wakizozana tarehe 10 Januari 2021.


Bi Passari aliripoti kisa hicho kwa polisi mwezi uliofuata lakini hakutoa malalamiko rasmi.Wanandoa hao walipatana na kuanza tena uhusiano, lakini baada ya kutengana, Bi Passari aliwasilisha malalamiko rasmi mnamo Desemba 2021.


Wakili Michael Kukulies-Smith alidai kuwa Bw Kyrgios alikuwa akijaribu kusitisha vita kwa kupiga simu Uber, na alikuwa amejaribu mara kwa mara "kisheria" kumhamisha Bi Passari mbali na gari kabla ya tukio hilo.


"Ni katika muktadha huo na mfadhaiko uliotokea, mteja wangu alijibu na kosa likatokea," alisema.

Post a Comment

0 Comments