Rais wa zamani wa Pakistan Jenerali Pervez Musharraf afariki dunia

 


Rais wa zamani wa Pakistan Jenerali Pervez Musharraf, ambaye alichukua mamlaka katika mapinduzi mwaka 1999, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.


Kiongozi huyo wa zamani - ambaye alikuwa rais kati ya 2001 na 2008 - alifariki huko Dubai baada ya kuugua kwa muda mrefu.


Alikuwa amenusurika majaribio mengi ya mauaji, na akajikuta yuko mstari wa mbele wa mapambano kati ya wanamgambo wa Kiislamu na nchi za Magharibi.


Aliunga mkono "vita dhidi ya ugaidi" vya Marekani baada ya 9/11 licha ya upinzani wa ndani.

Post a Comment

0 Comments