Sadio Mane arejea tena mazoezini na Bayern Munich

 


Mchezaji Sadio Mane amerejea tena mazoezini na timu yake ya  Bayern Munich baada ya kuuguza jeraha la mguu lililomfanya nahodha huyo wa Senegal kukosa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar.


Mane alipata jeraha hilo wakati wa ushindi wa bao 6-1 dhidi ya Werder Bremen kwenye ligi ya Bundesliga tarehe 8 Novemba mwaka jana.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye alijiunga na Bayern kutoka Majogoo wa Uingereza Liverpool msimu uliopita wa joto, baadaye alifanyiwa upasuaji na kuunganishwa tena kwenye sehemu ya juu ya mshipa wake wa kulia.

Post a Comment

0 Comments