Vita vya Ukraine: Urusi inapanga mashambulizi makali Februari 24, waziri wa ulinzi wa Ukraine asema

 


Waziri wa ulinzi wa Ukraine amesema Urusi inatayarisha mashambulizi mapya makubwa na kuonya kuwa huenda yakaanza tarehe 24 Februari.


Oleksii Reznikov alisema Moscow imekusanya maelfu ya wanajeshi na inaweza "kujaribu kitu" kuadhimisha kumbukumbu ya uvamizi wa awali mwaka jana.


Shambulio hilo pia lingeadhimisha Siku ya Watetezi wa Nchi ya Urusi mnamo tarehe 23 Februari, ambayo inaadhimisha mafaniko ya jeshi.


Wakati huohuo, watu watatu wamefariki katika shambulizi katika mji wa Kramatorsk.


Wengine wanane walijeruhiwa katika mji huo katika mkoa wa Donetsk baada ya kombora la Urusi kushambulia jengo la makazi, gavana wa mkoa alisema.


Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka huku waokoaji wakipitia mabaki hayo.


"Njia pekee ya kukomesha ugaidi wa Urusi ni kuushinda," Bw Zelensky aliandika kwenye mtandao wa kijamii kuhusu shambulio hilo. "Kwa mizinga. Ndege za kivita. Makombora ya masafa marefu."


Hivi majuzi Ukraine imetoa wito kwa ndege za kivita kusaidia kujikinga na mashambulizi ya anga baada ya Ujerumani, Marekani na Uingereza kukubali kupeleka vifaru.


Bw Reznikov alisema Moscow ilikuwa imekusanya wanajeshi 500,000 kwa ajili ya mashambulizi hayo.


Mnamo Septemba, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza uhamasishaji wa jumla wa askari 300,000 walioandikishwa, ambayo alisema ilikuwa muhimu ili kuhakikisha "hadhi ya nchi’


Lakini Bw Reznikov alipendekeza kuwa takwimu halisi iliyosajiliwa na kupelekwa Ukraine inaweza kuwa kubwa zaidi.


"Rasmi walitangaza 300,000 lakini tunapoona wanajeshi kwenye mipaka, kulingana na tathmini zetu ni zaidi," aliuambia mtandao wa BFM wa Ufaransa. BBC haiwezi kuthibitisha takwimu hii kwa njia uhuru.


Licha ya mapigano makali katika eneo la mashariki la Donbas, vita hivyo vimeingia katika hali ya mkwamo katika miezi ya hivi karibuni tangu Ukraine kutwaa tena mji wa kusini wa Kherson.


Isipokuwa kuchukuliwa kwa mji wa Soledar na Warusi hakuna upande ambao umepiga hatua kubwa kutwaa maeneo vitani

Post a Comment

0 Comments