Wagonjwa wa moyo na sukari waongoza

 


Zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa wanaofika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwananyamala wanasumbuliwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza huku magonjwa ya moyo na kisukari yakiongoza kwa kuwapata wagonjwa hao.


Hayo yamebainishwa na Daktari wa tiba kitengo cha magonjwa ya ndani Dkt Lilian Mjidange, na kusema imechangiwa na wananchi wenyewe kutokuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara hali inayochangia wanapofika hospitalini hapo ugonjwa unakuwa umeshakua mkubwa.


Amesema ili kukabiliana na tatizo hilo wananchi wenyewe hawana budi kubadilisha mtindo wa maisha wanayoishi kwa sasa kwani ndio chanzo cha kuwepo kwa idadi kubwa ya wagonjwa wenye magonjwa hayo yasiyo ya kuambukiza.


Kwa upande wao wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wameomba elimu juu ya masuala ya lishe itolewe kwa wananchi mara kwa mara huku wakieleza kwamba hali ngumu ya maisha nayo imekuwa ikichangia watu kula vyakula vinavyohatarisha usalama wa afya zao.

Post a Comment

0 Comments