Wanandoa wanaocheza densi wa Iran wahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela

 


Wanandoa wa Iran walio na umri wa miaka 20 wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kuchapisha video yao wakicheza dansi mitaani.


Inasemekana walitiwa hatiani kwa kuendeleza ufisadi, ukahaba na propaganda.


Video hiyo iliwaonyesha wakicheza katika Mnara wa Azadi (Uhuru) wa Tehran.


Mamlaka zinatoa hukumu kali kwa watu wanaoonekana kuhusika na maandamano baada ya kifo cha mwanamke ambaye alizuiliwa na polisi wa maadili.


Wanandoa hao hawakuhusisha ngoma yao na maandamano yanayoendelea nchini Iran.


Chanzo kimoja kimeithibitishia BBC Monitoring kwamba kukamatwa kwa wapenzi hao kulitokea baada ya kuweka video hiyo kwenye akaunti zao za Instagram, ambazo kwa pamoja zina wafuasi karibu milioni mbili.


Maandamano ya kuipinga serikali - yaliyoitwa "machafuko" na utawala wa Iran - yalienea kote nchini baada ya Mahsa Amini, 22, kufariki akiwa mikononi mwa polisi Septemba mwaka jana.Alikamatwa mjini Tehran kwa madai ya kukiuka sheria ya kuwataka wanawake kufunika nywele zao na hijabu, au hijabu.


Astiazh Haqiqi, 21, na mchumba wake Amir Mohammad Ahmadi, 22, wanasemekana kutiwa hatiani kwa "kukuza ufisadi na ukahaba, kushirikiana dhidi ya usalama wa taifa, na propaganda dhidi ya utawala huo".


Nyumba ya familia ya Bi Haqiqi, ambaye anaorodhesha taaluma yake kama mbunifu wa mitindo, ilivamiwa kabla ya kukamatwa.


Haijulikani hukumu hiyo ni ya muda gani kwa kila moja ya hukumu tofauti zinazowakabili.Wamehukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka 10 na nusu - kifungo cha pamoja kwa mashtaka hayo.


Ikiwa maamuzi yao yatazingatiwa, watalazimika kutumikia kifungo kirefu zaidi kati ya masharti hayo ya hukumu.


Kulingana na ripoti, pia walipewa marufuku ya miaka miwili ya kutumia mitandao ya kijamii na kuondoka nchini.

Post a Comment

0 Comments