Wezi wa mafuta ya SGR watiwa mbaroni


Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewakamata watu wanne wanaodaiwa kupokea na kuuza mali ya wizi ikiwa ni pamoja na mafuta ya dizeli lita 850 ambayo yanadaiwa kuibwa kwenye ujenzi wa kisasa wa SGR, pikipiki, mapipa, madumu na mipira vilivyokuwa vinatumia silaha na kuhifadhi mafuta.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amewataja watu hao kuwa ni Wilbert Costantine, Mihambo Elias, Paschal Abdalah na Steven Jacob.


Amesema kukamatwa kwa watu hao kunatokana na oparesheni iliyoanza mwanzoni mwa huu hasa katika maeneo inayopita reli hiyo ya kisasa, ambapo jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata hao huku wengine wakiendelea kusakwa.


'Sasa bwana huyu tumempeta pamoja na kwamba alikuwa anajificha muda mrefu kwa kuhama hama lakini pia tarehe 4 mwezi wa pili mwaka huu katika Kijiji cha Mantare tarafa ya Ngula wilayani Kwimba tulikamatwa madumu 16 yenye mafuta ya dizeli yakiwa yamefichwa kwenye shamba la mahindi la bwana mmoja anayeitwa. Safari Peranya huyu bwana alikimbi bado tunamtafuta na tutamkamata na kumuwajibisha kuhifadhi mali ya wizi'


Katika hatua nyingine kamanda Mutafungwa amesema Kijiji cha Hundya Kwimba alikamatwa mpokeaji wa mafuta Paschal Abdalah ana miaka 20 ni msukuma mkazi wa mkoa wa Shinyanga akiwa na pikipiki iliyobeba mafuta dizeli lita 190  


Kamanda Mutafungwa amewaonya mradi huo wasio waaminifu na kusema wakibainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Post a Comment

0 Comments