https://monetag.com/?ref_id=TTIb Hati ya kukamatwa kwa Putin: Biden apongeza hatua ya kufunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita ya ICC | Muungwana BLOG

Hati ya kukamatwa kwa Putin: Biden apongeza hatua ya kufunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita ya ICC

 


Rais wa Joe Biden amepongeza sheria ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) uliotoa hati ya kukamatwa kwa mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin.


Mahakama ya ICC ilimshutumu Rais Putin kwa kufanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine - jambo ambalo Rais Biden alisema kiongozi huyo wa Urusi "alifanya kwa uwazi".


Madai hayo yanaangazia uhamishaji haramu wa watoto kutoka Ukraine hadi Urusi tangu uvamizi wa Moscow mwaka 2022.


Moscow ikakanusha madai hayo na kushutumu vibali hivyo kuwa vya "kuudhi".


Kuna uwezekano mkubwa kwamba hakuna mengi yatakayotokea, kwani ICC haina mamlaka ya kuwakamata washukiwa bila ushirikiano wa serikali ya nchi.


Urusi si nchi mwanachama wa ICC, maana yake mahakama hiyo haina mamlaka hapo.


Hata hivyo, inaweza kumuathiri Bw Putin kwa njia zingine, kama vile kutoweza nje kwa sababu sasa anaweza kukamatwa ikiwa atakanyaga katika nchi yoyote kati ya 123 wanachama wa mahakama hiyo.


Bw Putin ni rais wa tatu kupewa hati ya kukamatwa na mahakama ya ICC.


Rais Biden alisema kuwa, wakati mahakama pia haikuwa na mamlaka nchini Marekani, utoaji wa kibali hicho "hutoa maana kubwa sana".


Utawala wake ulikuwa tayari "umeamua rasmi" kwamba Urusi ilifanya uhalifu wa kivita wakati wa mzozo unaoendelea nchini Ukraine, huku Makamu wa Rais Kamala Harris akisema mnamo Februari kwamba wale waliohusika "watawajibishwa".


Umoja wa Mataifa pia ulitoa ripoti mapema wiki hii ambayo iligundua kitendo cha Moscow kuwaondoa watoto wa Ukraine kwa lazima na kupeleka katika maeneo yaliyo chini ya mamlaka yake na kutambua kuwa sawa na uhalifu wa kivita.


Katika taarifa yake siku ya Ijumaa, ICC ilisema ina sababu za kuridhisha za kuamini kuwa Bw Putin alitenda uhalifu huo moja kwa moja, pamoja na kufanya kazi na wengine.


Pia ilimshutumu kwa kutumia mamlaka yake ya urais kuzuia watoto nchini humo lazima.

Post a Comment

0 Comments