Kimbunga chaua 23 usiku wa kuamkia leo Mississippi Marekani

 


Takriban watu 23 wamefariki dunia baada ya kimbunga kukumba jimbo la Mississippi nchini Marekani usiku wa kuamkia leo. Watu zaidi wanadhaniwa wamenaswa chini ya vifusi vya majengo yaliyoharibiwa.


Kimbunga hicho kilisababisha uharibifu mkubwa katika miji kadhaa ya mashambani, ambapo miti na nyaya za umeme zilikatwa na makumi ya maelfu ya kukatika kwa umeme kuripotiwa.


Majimbo mengine kadhaa ya kusini pia yanakabiliwa na dhoruba kali. Mvua ya mawe ukubwa wa mipira ya gofu na mvua kubwa iliripotiwa katika maeneo kadhaa ya jimbo. Wakazi wa Rolling Fork, mji mdogo ulioko magharibi mwa Mississippi, walisema kuwa kimbunga kilipeperusha madirisha ya nyumba zao.


Uharibifu katika eneo hilo unaripotiwa kuwa mbaya haswa.


Mkazi wa eneo hilo Brandy Showah aliiambia CNN: "Sijawahi kuona kitu kama hiki... Huu ulikuwa mji mdogo sana, na sasa umetoweka." Cornel Knight aliambia shirika la habari la Associated Press kwamba yeye, mke wake na binti yao mwenye umri wa miaka mitatu walikuwa katika nyumba ya jamaa huko Rolling Fork na kwamba ilikuwa "shwari" kabla ya kimbunga hicho kupiga.

Post a Comment

0 Comments