Nato yalaani matamshi "hatari" ya nyuklia ya Urusi

 


Nato imelaani matamshi "hatari" na "ya kutowajibika" ya Urusi baada ya uamuzi wa Vladimir Putin wa kuweka silaha za nyuklia huko Belarusi.


Shirika hilo "linafuatilia kwa karibu" hali hiyo na kusema kuwa hatua hiyo haiwezi kuliongoza kubadili mkakati wake wa nyuklia.


Marekani ilisema haiamini kuwa Urusi inajiandaa kutumia silaha za nyuklia.


Belarus inapakana kwa sehemu kubwa na Ukraine, pamoja na wanachama wa Nato Poland, Lithuania na Latvia.


Ukraine imeitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kushughulikia tishio linaloweza kusababishwa na tangazo la Rais Putin siku ya Jumamosi.


Rais Putin alisema Moscow haitakuwa ikihamisha udhibiti wa silaha zake kwa Minsk na kwamba kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko - mshirika mkubwa wa Kremlin na mfuasi wa uvamizi wake wa Ukraine - alikuwa amezungumzia suala hilo kwake kwa muda mrefu.


Ukraine inasema hatua hiyo inakiuka makubaliano ya kutosambaza silaha za nyuklia - tuhuma ambayo Rais Putin amezikanusha, badala yake anailinganisha na Marekani kuweka silaha zake barani Ulaya.


Lakini Nato siku ya Jumapili ilielezea kurejelea kwa Urusi kuhamisha silaha za nyuklia kama hatua ya "kupotosha".


Muungano huo wa kijeshi pia uliishutumu Urusi kwa kuvunja mara kwa mara ahadi zake za udhibiti wa silaha, ikiwa ni pamoja na uamuzi wa nchi hiyo kusitisha mkataba mpya wa START - mkataba uliotiwa saini mwaka 2010 ambao unaweka kikomo idadi ya vichwa vya nyuklia vya Marekani na Urusi na kila mmoja ana uwezo wa kukagua makubaliano ya mwenzake.


Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell aliitaka Belarus kujiondoa katika makubaliano hayo na Putin, akionya kuwa nchi hiyo inaweza kukabiliwa na vikwazo zaidi ikiwa itautekeleza

Post a Comment

0 Comments