https://monetag.com/?ref_id=TTIb Spurs yaachana na Conte kusaka kocha wanne ndani ya miaka 4 | Muungwana BLOG

Spurs yaachana na Conte kusaka kocha wanne ndani ya miaka 4

 


Meneja Antonio Conte ameachana na Tottenham Hotspur kwa makubaliano maalumu baada ya kuiongoza timu hiyo kwa miezi 16.


Conte aliwaita wachezaji wa Spurs "wabinafsi" na kukosoa utamaduni wa klabu hiyo kupitia mkutano na waandishi wa habari baada ya timu yake kwenda sare ya hivi majuzi dhidi ya Southampton.


Tottenham wako katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi lakini wametolewa katika mashindano mengine yote ya kuwania vikombe.


Msaidizi wa Conte Cristian Stellini atashika mikoba na kuwa kocha mkuu wa muda mpaka mwisho mwa msimu, huku kiungo wa zamani Ryan Mason akiwa msaidizi wake.


"Tumebakiza mechi 10 za ligi kuu England na tunapambana kuwania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya," mwenyekiti Daniel Levy alisema.


"Sote tunahitaji kuwa wa moja. Kila mmoja anapaswa kujitokeza ili kuhakikisha tunamaliza nafasi za juu kabisa kwa ajili ya klabu na mashabiki zetu waaminifu."


Kuondoka kwake kunamaanisha kuwa Spurs wanasaka kocha wao wanne wa kudumu katika kipindi cha miaka minne tangu Mauricio Pochettino aondoke mwaka 2019.

Post a Comment

0 Comments