Usambazaji wa nyaya za data za ulimwengu: Mradi huu kuziingiza China na Marekani katika 'vita ya teknolojia'?

 


Nyaya ama kebo za chini ya bahari, ambazo hubeba data za ulimwengu, sasa ni msingi wa vita vya teknolojia kati ya Marekani na China.


Washington, inayohofia majasusi wa Beijing, imezuia miradi ya Wachina nje ya nchi na kuziba njia za waya za Big Tech hadi Hong Kong, Reuters imebaini.


Ilianza kama biashara madhubuti: mkataba mkubwa wa kibinafsi wa kupitisha nyaya za mtandao chini ya bahari. Ikaleta uhasama katika vita vya wakala kutoka Marekani na China juu ya teknolojia hiyo ambayo inaweza kuamua ni nani atakayetawala kiuchumi na kijeshi katika miongo kadhaa ijayo.


Mnamo Februari, kampuni ya usambazaji nyaya za chini ya bahari ya Marekani ya SubCom LLC ilianza kuweka nyaya ama kebo kwa mradi wa thamani ya dola $600-milioni ili kusafirisha data kutoka Asia hadi Ulaya, kupitia Afrika na Mashariki ya Kati, kwa kasi ya juu zaidi ya maili 12,000 za nyuzinyuzi zinazopita kwenye sakafu ya bahari.

Post a Comment

0 Comments