Mwenyekiti Mbowe ametoa rai hiyo wakati alipohutubia mkutano wa hadhara, Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
"Mataifa yanayojitambua duniani hayapimi utajiri wake kwa kuhesabu madini, hayapi utajiri wake kwa hesabu misitu na mbuga za wanyama. Yanapima utajiri kwa namna nchi imewekeza akili kwa watu wake.
Akizungumzia kuhusu Uchaguzi ujao, Kiongozi huyo amesema bado wanaendelea kuona maridhiano yatakapowapeleka na kwamba sasa wanaangalia sheria za uchaguzi pamoja na Tume ya uchaguzi.
0 Comments