VIDEO: Polisi wakamata Bastola na risasi 71


Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kukamata bastola moja aina ya CZ 75 LUGER
yenye namba za usajili A487385 pamoja na risasi 71 za bastola iliyokuwa inatumiwa na
wahalifu.

Akitoa taarifa hiyo leo Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP
Justine Masejo amesema silaha hiyo pamoja na risasi zilipatikana katika nyumba iliyopo huko
maeneo ya Ilkyurei, Kata ya Kiranyi, wilaya ya Arumeru na mkoa wa Arusha.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Post a Comment

0 Comments