https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wanne washirikiana kumuua dada yako kisa ardhi | Muungwana BLOG

Wanne washirikiana kumuua dada yako kisa ardhi

 


Wanafamilia wanne wilayani Rukiga nchini Uganda wamekamatwa kwa madai kuwa walimshambulia dada yao hadi kufa kufuatia mvutano wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.


Jana, msemaji wa polisi mkoa wa Kigezi, Elly Maate, alimtaja marehemu kuwa ni Christine Kiconco mwenye umri wa miaka 41 huku watuhumiwa hao ni Innocent Tumwekwase, Samuel Atuhirwe, Christopher Bikorwomuhangi na Justus Mayumba.


Marehemu na watuhumiwa wote ni wakazi wa Kiini cha Rwenderema, Parokia ya Ibumba iliyopo Kata ndogo ya Rwamucucu, Wilaya ya Rukiga.


"Inadaiwa kuwa familia ya marehemu imekuwa na matatizo ya kinyumbani yanayotokana na ardhi ambayo iligawanywa miongoni mwa watoto na baba yao Selestino Byaruhanga," alisema Maate.


"Wavulana hao waliuza mara moja uwanja waliopewa awali na kuanza kudai sehemu ambayo walipewa wasichana na tangu wakati huo, wamekuwa wakimtishia marehemu," aliongeza.

Post a Comment

0 Comments