Maisha ya raia wa Uingereza yamo hatarini kutokana na kuvuja kwa taarifa za marekani za ujasusi, limeandika gazeti la Times nchini Uingereza, likiinukuu Kamati ya Ulinzi ya bunge la Uingereza.
Awali, vyombo vya habari viliripoti kuwa kuvuja kwa waraka tarehe 23 Machi, ambao ulidai kwamba v wanajeshi wa kikosi maalumu wa Uingereza hadi 50 walitumwa nchini Ukraine pamoja na vikosi vingine maalum kutoka nchi za Magharibi.
Waraka huo hauonyeshi ni wapi vikosi hivi vilipo na ni nini vinafanya.
"Sehemu kubwa ya maudhui ya ripoti hizi ni uongo, zimebadilishwa, au zimefanyiwa yote ," Times lilimnukuu msemaji wa wizara ya ulinzi ya Uingereza "Tunashauri kwamba mtu yeyote asichukulie kwa umakini madai haya kuwa yenye thamani."
Huku Pentagon ikijaribu kutafuta chanzo cha uvujaji mkubwa wa taarifa zake za siri, maafisa wa Uingereza, wa kijeshi na ujasusi hawachukulii kirahisi uvujaji wa taarifa hizi.
"Pentagon haijui ni nini kingine kinaweza kutokea," chanzo cha usalama kililiambia gazeti la Times. "Inatia wasi wasi kusema kweli, na kunaweza kuwa na uvujaji zaidi kabla ya kufichwa."
Kamanda wa kikosi maalumu cha zamani na ambaye kwa sasa ni mbunge wa chama cha LabourDan Jarvis aliliambia gazeti kwamba operesheni ya aina hiyo inayohusisha kikosi maalumu cha Uingereza kwa kawaida huwa ininafanyika kwa siri.
"Kupatikana kokote kwa taarifa za siri kuhusiana na mahala walipo au idadi yo, sio jambo linaloaibisha tu , bali ni hasara kijeshi. Inahatarisha usalama na ufanisi wa operesheni hizi na inaweza kuyaweka maisha hatarini," alisema.
0 Comments