Watu 13 waliotambulika kuwa ni wafanyabiashara wamefariki dunia Kwa ajali ya barabarani usiku wa kuamkia leo walipokuwa wakisafiri na gari la mnada katika Kijiji cha Namatuhi Wilayani Songea Mkoani Ruvuma walipokua wakitokea eneo la Ndongosi Mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma ACP Marco Chilya amesema ajali hiyo imetokea katika daraja la mto Njoka kata ya Namatuhi halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma majira ya saa tatu usiku.
Kamanda ACP MARCO CHILYA ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo ilisababisha gari hilo aina ya Fuso kupinduka na kuangukia mtoni na kusababisha vifo 13 vya wafanyabiashara hao.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE
0 Comments