Taasisi ya Dini ya Kiislam ya Al- Hikma Foundation ya Jijini Dar es salaam, imetanganza kuwaozesha Vijana 50 kwa kuwalipia mahari ambao bado hawajaoa kutokana na changamoto za kifedha na wapo tayari kutekeleza Ibada ya ndoa.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Sheikh Nurdini Kishki ameleeza hayo wakati wa Mashindano ya 23 ya Kimataifa ya kuhifadhi Qur’aan Tukufu yaliyofanyika leo April 09 2023, Uwanja wa Uhuru Dar es salaam, yakihudhuriwa na Viongozi wa Serikali na Kidini huku Mgeni rasmi katika mashindano hayo akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE
0 Comments