Aliyezuia polisi mahakamani ni wakili feki - TLS


Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kimesema kuwa Baraka Mkama ambaye alitambulika kama wakili na kuonekana akiwazuia askari Polisi wasiwatie nguvuni wateja wake baada ya kuachiwa huru na Mahakama sio wakili wala chama cha TLS.


Taarifa ya TLS imeeleza kuwa baada ya tukio hilo uongozi wa TLS uliunda kamati ya uchunguzi wa tukio hilo na baada ya uchunguzi wamebaini mtu huyo sio wakili.


Baada ya kupokea taarifa ya kamati, Baraza la Uongozi la TLS lilipitia na kuijadili, kwa hivyo, tunapenda kuwafahamisha Wanachama wote wa TLS, Wadau wa TLS na Umma wa Watanzania kwamba, TLS tumejiridhisha pasipo shaka kwamba mhusika wa tukio hilo ndugu Baraka Mkama sio wakili na sio mwanachama wa tanganyika law society.


Aidha TLS imeeleza kuwa imepata taarifa muhimu za ziada kuhusu mtandao wa watu wasiokuwa mawakili wanaofanya kazi za uwakili (Vishoka) hivyo imeongezea muda Kamati Teule ya ujao ujao na kuwasilisha taarifa zake za ziada ifikapo tarehe 31 Mei 2023


Vilevile, TLS imekamilisha kuunda kikosi kazi (Anti-Vishoka Taskforce) kitakachofanya kazi ya watu ambao hawastahili kufanya kazi za mawakili. Baraza la Uongozi la TLS linaomba toka kwa Wanachama wa TLS, Wadau wa TLS na Wananchi katika juhudi za kutokomeza uhalifu huu. 


TLS inawakumbusha wananchi na wadau wake wote kila wakati kuhakiki taarifa za watu wanaoruhusiwa kufanya kazi za mawakili kwa kutumia mfumo wa wakili wa Mahakama yaani e-wakili. TLS itahakikisha kuwa inalinda na maslahi ya mawakili; itawalinda na kuwatetea wananchi dhidi ya vishoka; na vyombo vya dola katika mamlaka hadhi, nidhamu na heshma ya Mawakili kama mamlaka ya Mahakama wakati wote.

Post a Comment

0 Comments