https://monetag.com/?ref_id=TTIb ‘Mackenzie alitumia genge lililojihami kwa silaha kuwaua waumini waliochukua muda mrefu kuaga dunia’ - Waziri | Muungwana BLOG

‘Mackenzie alitumia genge lililojihami kwa silaha kuwaua waumini waliochukua muda mrefu kuaga dunia’ - Waziri

 


Kiongozi wa wa kanisa la kufunga hadi kufa huko Kilifi Paul Mackenzie alitumia genge lililomiliki vifaa butu kuwaua baadhi ya waumini waliochukua muda mrefu kufa na wale waliobadilisha mawazo yao wakati wa kufunga , alisema Waziri wa masuala ya ndani nchini Kenya Kindiki Kithure.


Kiongozi huyo anasema magenge hayo yaliomiliki silaha yalijenga vibanda karibu na makaburi ya waliofariki na kula chakula cha lishe bora huku wakiwataza waumini waliokufa njaa.


Ugunduzi wa makaburi ya halaiki mwezi uliopita umelishangaza taifa katika kile kilichotajwa kuwa mauaji ya msitu wa Shakahola.


Maafisa wa polisi wanaamini kwamba miili mingi ni ya waumini wa kanisa la Mackenzie anayedaiwa kuwaagaiza kufunga hadi kufa.


Huku njaa ikidaiwa kuwa chanzo kikuu cha vifo hivyo, baadhi ya waathiriwa wakiwemo Watoto , walinyongwa , kupigwa hadi kufa, kufunikwa pua na mdomo, kulingana na mwanapatholojia mkuu Johannsen Oduor.

Post a Comment

0 Comments