Marekani yawawekea vikwazo makamanda wa Al-Shabaab wa Somalia

 


Marekani imewalenga makamanda wa ngazi ya kati wa al-Shabab na maafisa wa ngazi ya chini wa fedha kwa vikwazo vipya.


Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliwaorodhesha makamanda watano wa kundi hilo la wanamgambo wa Somalia kuwa magaidi wa kimataifa, huku wizara ya fedha ya Marekani ikiwaorodhesha watu na mashirika 26, wakiwemo wasafirishaji wa makaa.


Wanne kati ya watano waliowekewa vikwazo wanatuhumiwa kuhusika katika kukusanya kodi kwa niaba ya al-Shabab na kutekeleza mashambulizi dhidi ya raia na vikosi vya Somalia.


Marekani iliripoti kwamba al-Shabab hupata takriban dola milioni 100 kila mwaka ambazo hukusanywa kupitia kodi haramu, michango ya lazima na ulafi.


Miongoni mwa watendaji walioorodheshwa hivi karibuni ni Mohamed Siidow, ambaye anaelezewa kama kiongozi wa kifedha na kamanda wa kitengo cha kijeshi cha al-Shabaab cha Jabha.


Anadaiwa kusimamia shughuli za kutoza kodi haramu katika kijiji cha Aliyow Barrow eneo la Lower Shabelle.

Post a Comment

0 Comments