Polisi wamsaka aliyemjeruhi mke wake Arusha

 


Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Justin Masejo amesema wanamtafu Isaack Mnyagi mkazi wa Sombetini jijini.


Arusha anayetuhumiwa kumpiga mwenza wake, Jackline Mnkonyi (38) na kisha kumng'oa jino la mbele na kumtoboa jicho.


Tukio hilo limetokea juzi Alhamisi Mei 25, 2023 baada ya kutokea ugomvi ambao unadaiwa kuchangiwa na wivu wa mapenzi baina ya wenzao.


Jackline ambaye anamtoto mchanga amesema amepigwa na mumewe baada ya kumtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mgeni aliyefika nyumbani bila kujua Kama ni mjomba wake.


"Nilijitahidi sana kujieleza lakini ilishindikana alianza kunipiga mateke na ngumi na alichukua Praizi na kuniamuru nifungue mdomo na kuning'oa jino moja ambapo damu zilianza kuchuruzika,"amesimulia kwa uchungu huku akilia.

Post a Comment

0 Comments