Senegal: Wafuasi wa Sonko wakabiliana na polisi

 


Makabiliano yalizuka Ijumaa usiku kati ya polisi na wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, wakato msafara wake wa magari ulipowasili mjini Kolda, kusini mwa nchi hiyo.


Sonko alikuwa akisafiri kuelekea mji mkuu wa Dakar, ambako anatarajiwa kufika mahakamani ijayo kujibu mashtaka ya ubakaji na kutoa vitisho vya mauaji.


Amekanusha mashtaka dhidi yake na huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani endapo atapatikana na hatia.


Sonko hivi karibuni alikuhumiwa kifungo cha miezi sita bila ya kuzuiliwa gerezani, na alitangaza kwamba hataendelea kuheshimu amri za kutakiwa kufika mahakamani.


Wafuasi wake wameitisha maandamano kupinga kesi dhidi ya Sonko, wanazosema kwamba zina ushawishi wa kisiasa ili kumzuia asigombee urais katika uchaguzi mkuu wa ujao 2024.


Sonko alikuwa amebadilisha safari yake ya kilomita 500 kuwa msafara wa magari aliouita kuwa wa uhuru, akitoa wito kwa wafuasi wake kumfuata mji wa nyumbani kwake wa Ziguinchor, kusini mwa Senegal, hadi mji mkuu Dakar.


Serikali imeapa kwamba itakabiliana na tukio lolote litalotaka kuathiri na amani.

Post a Comment

0 Comments