F Mwanamke ajiua baada ya kukiri kumsaliti mume wake | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mwanamke ajiua baada ya kukiri kumsaliti mume wake


Salma Shaibu (28) kutoka Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, amefariki dunia baada ya kujiua kwa kunywa sumu ya wadudu huku ikidaiwa kuwa chanzo cha kifo chake ni kuji kuwa mwenye hatia baada ya kukiri mwenyewe kuwa alichepuka na mwanaume mwingine


Inaelezwa ya kwamba, Marehemu Salma Shaibu enzi za uhai wake alikuwa akiishi na Mumewe Ramadhani Hamisi Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.  


Taarifa zinaeleza kuwa aliwahi kusafiri kuelekea wilayani Newala-Mtwara na huko inaaminiwa alishawishika na kuingia kwenye mahusiano na Mwanaume mwingine. 


Baada ya kurudi nyumbani kwa Mumewe Masasi, Salma hakuwa na furaha na katu hakulia kilichomsibu na baada ya kusimulia aliamua kujiua. 


Kutokana na fedheha hiyo kumkera moyoni mwake, aliamua kumsimulia rafiki yake wa kike na mdogo wake lakini wote walimpa moyo na kumwambia akae kimya kwani jambo hilo akilisikia mumewe kuzua balaa. Baada ya kurudi kwa mumewe aliendelea kuonekana mwenye simanzi kubwa, licha ya kuulizwa na mumewe mara kadhaa ni kipi kinamsibu, katu hakumweleza ukweli.


Baadae bwana Ramadhani aliamua kumuuliza rafiki wa mkewe kwanini mkewe ana huzuni tele, rafiki wa marehemu alimsimulia mume wa Salma yote yaliyojiri baada ya rafiki yake kuchepuka, jambo ambalo halikumshtua mume huyo na kukiri kuwa hilo ni jambo la kawaida na kukiri kuongea na mke wake ili. kulimaliza tatizo hilo.


Inasemekana ya kwamba, licha ya Mume kujaribu kumuweka sawa mke na kumuambia kuwa ni jambo la kawaida kwani hata yeye kuna wakati hakuwa mwaminifu, marehemu alionekana bado mwenye furaha na ndipo alipoaga kwenda Wilayani Nachingwea kumsalimia baba yake mgonjwa.


Baada ya kufika Nachingwea, alikaa siku mbili na kuamua kunywa sumu kali ya kuulia wadudu kwenye mikorosho. zinasema, Mwili wa Marehemu Salma ulikutwa pamoja na karatasi yenye ujumbe unaosema nimeshindwa kwa makosa yangu mwenyewe huku mkononi mwake akiwa ameandika ujumbe ambao unaendana kuona na maneno aliyoyaandika kwenye karatasi na kusisitiza sio tatizo la yeyote, bali ni ujinga wake na kujihisi ameikosea familia na Mungu wake.


Baada ya Mwili wa Marehemu kufikishwa kwenye Hospitali ya Misheni ya Mnero, Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, imebainika kuwa alifariki baada ya sumu aliyokunywa kuathiri viungo vya ndani ya mwili na mfumo wa upumuaji jambo lililosababisha umauti kwa mwanamke huyo.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Lindi Pili Mande, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa vijana kushirikisha watu mbalimbali kuhusu masuala yanayowahusu na kupata ushauri wa kutatua huku akiwaelekeza dawa la Jinsia jeshi hilo kuelezea changamoto mbalimbali za mahusiano ili kupata msaada na kuepusha maamuzi magumu ya kujiua.


Marehemu Salma Shaibu, ameacha watoto wawili ambapo mkubwa ameanza kusoma elimu ya awali, Leo tarehe 14 mwezi Juni, amefikishwa kwenye makazi ya milele baada ya kufariki siku ya tarehe 13 mwezi Juni mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments