F Kanisa la KKKT kujenga ghorofa kubwa la kitega Uchumi Mbulu. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kanisa la KKKT kujenga ghorofa kubwa la kitega Uchumi Mbulu.





Jengo kubwa la Kitega uchumi linalojengwa na kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania jimbo la Mbulu.

Jiwe la Msingi katika jengo kubwa la kitega uchumi la Kanisa la KKKT Mbulu.
Baba Askosu Dr. Alex Malasusa akizungumza na waumini wa kanisa hilo na watu wengine wakati wa ibada ya kuweka jiwe la msingi jengo la kitega uchumi Mbulu.

Na John Walter-Manyara    

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)  Baba Askofu Dkt.Alex Malasusa ameweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo kubwa la kitega uchumi cha kanisa hilo wilayani Mbulu mkoani Manyara.

Baba Askofu Alex Malasusa aliongoza waumini wa kanisa hilo na watu wengine kwenye Harambee ya ukamilishaji wa  ujenzi  wa jengo hilo ambayo ilisaidia kupatikana shilingi Milioni 12,500,000.

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Kheri amelipongeza kanisa hilo kwa kuiunga mkono serikali katika uwekezaji kwani utachochea maendeleo na Uchumi wa Mbulu.     

James ameeleza kuwa mahusiano ya Serikali na madhehebu ya Dini wilayani humo ni mazuri na yamekuwa ni Msingi wa ushirikiano katika sekta ya Elimu, Afya, usimamizi wa maadili na vita dhidi ya ukatili wa kijinsia.             

Naye Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mbulu Baba Askofu Nicholas Nsangenzelu amewashukuru Wananchi na watumishi wote na kipekee Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono uwekezaji huo muhimu kwa kuchangia pamoja na Wananchi wengine.



Post a Comment

0 Comments