Ukraine yasema mustakabali wa unategemea mashambulizi ya ndege zisizo na rubani

 


Fedorov alisema uzalishaji wa ndege zisizo na rubani za Ukraine umeongezeka kwa zaidi ya mara 100 tangu mwaka jana.


Waziri anaesimamia Mabadiliko ya Kidijitali nchini Ukraine Mykhailo Fedorov aliiambia shirika la habari la Reuters kwamba mustakabali wa vita vya Ukraine dhidi ya Russia unategemea na mashambulizi mengi yatakayofanywa na ndege zisizo na rubani na kuwepo na mashambulizi machache ya meli Russia.


Fedorov alisema uzalishaji wa ndege zisizo na rubani za Ukraine umeongezeka kwa zaidi ya mara 100 tangu mwaka jana.


Fedorov pia aliliambia Reuters kwamba Ukraine inafanyia majaribio mifumo ya teknolojia ya AI, ambayo inaweza kutambua shabaha kwa umbali umbali wa kilomita kadhaa, pamoja na vifaa vinavyoongoza ndege zisizo na rubani licha ya kuharibiwa nmitambo ya kivita ya kielektroniki.


Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, katika taarifa zake za kijasusi za kila siku kuhusu Ukraine, ilisema kuna uwezekano kwamba Russia itaanza tena kutumia makombora ya masafa marefu ili kulenga miundombinu ya Ukraine wakati wa baridi.

Post a Comment

0 Comments