Wakili maalum amuomba jaji kumuwekea Trump amri kumnyamazisha


 Mwendesha mashtaka anayeongoza kesi ya kuingilia uchaguzi dhidi ya Donald Trump amemtaka jaji kumweka amri ya kukataza mawakili, wahusika, au mashahidi kuzungumza juu ya kesi hiyo kwa umma.


Wakili Maalum Jack Smith alisema kwamba amri "hiyo" ingezuia unyanyasaji wa mashahidi.


Bw Trump alijibu mtandaoni, akishutumu timu ya Smith kwa utovu wa nidhamu, akiandika: "hawataniruhusu KUONGEA?"


Trump amekana kuwa na hatia ya kula njama ya kutengua uchaguzi wa mwaka 2020.


Ombi hilo lilifunguliwa na Jaji wa Mahakama ya Wilaya Tanya Chutkan na kuwasilishwa wiki moja kabla. Ilikuwa miongoni mwa hati nyingi za mahakama kutoka kwa kesi hiyo ambazo zilitolewa Ijumaa.


Waendesha mashitaka wanasema agizo lao lililopendekezwa - ambalo hawalirejelei kamwe kama "amri ya zuio" - ni iliobainishwa vyema" ambayo ni muhimu kwenye kuzuia taarifa potofu, vitisho na "kuathiri" kesi hiyo.


Iwapo amri hiyo itaidhinishwa, itapiga marufuku Bw Trump kutoa matamshi "kuhusu utambulisho, ushuhuda, au uaminifu wa mashahidi watarajiwa" na "maelezo kuhusu upande wowote, shahidi, wakili, wafanyakazi wa mahakama, au majaji watarajiwa ambayo ni ya kudhalilisha, uchochezi, au kutisha" .


Haimuwekei vizuizi vyovyote kwa Bw Trump kunukuu kutoka kwa hati za rekodi za umma au kutangaza kuwa hana hatia.


Vizuizi vyovyote vilivyowekwa katika marekebisho ya kwanza ya rais huyo wa zamani juu ya uhuru wa kujieleza, haswa anapowania urais mwaka wa 2024, vitaanzisha pingamizi kubwa la kikatiba mahakamani.


Wiki iliyopita, mawakili wa Bw Trump walimwandikia Jaji Chutkan, wakisema kuwa ana upendeleo na kumtaka ajiepushe na kesi hiyo.

Post a Comment

0 Comments