Biden 'ana matumaini kidogo' kuhusu kuachiliwa kwa mateka wa Gaza

 


Rais wa Marekani Joe Biden anasema "ana matumaini kidogo" kuwa kutakuwa na mpango wa kuwakomboa zaidi ya watu 200 wanaoshikiliwa mateka Gaza.


Aliuambia mkutano na waandishi wa habari California hapo awali kwamba hakutaka kuzungumza kabla ya wakati wake lakini kwamba Marekani imeona "ushirikiano mkubwa" kutoka kwa Qatar, ambayo imekuwa ikiongoza mazungumzo yanayoendelea kati ya Israel na Hamas.


Akizungumzia operesheni ya hivi karibuni ya Israel katika hospitali kubwa zaidi ya Gaza - Al-Shifa - rais huyo wa Marekani anasema Hamas ilifanya "uhalifu wa kivita" kwa kuwa na kituo chini yake.


Israel imeonyesha kile inachodai kuwa ni silaha na vifaa vingine vya Hamas ambavyo vilipatikana kutoka hospitalini.


Hamas inakanusha kuwa inatumia vituo vya matibabu kama ngome ya harakati zake za kijeshi dhidi ya Israel.


Biden anasema Marekani imeitaka Israel kuwa makini , kuhakikisha kuwa raia wanakuwa salama wakati wa kuzisaka ngome za Hamas.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items