DC Kheri James ataka maarifa kutumika zaidi kutatua Migogoro.
Na John Walter-Mbulu

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Kheri James, ameeleza kuwa pamoja na jitihada kubwa zinazotumika kuwekeza katika elimu, lakini bado jamii inajukumu kubwa la kutambua umuhimu wa kuwatumia watu wenye maarifa katika kupanga, kuamua na kusaidia utatuzi wa mambo mbalimbali.               

Amesema hayo aliposhiriki Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Biblia ECLEA Tawi la Mbulu iliofanyika novemba 18 wilayani humo.                                   

Adha James ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kufungua Tawi katika wilaya ya Mbulu, na ameahidi kuwapa ushirikiano ili lengo na dhamira njema ya Chuo isikwame.                               

Pamoja na mambo mengine mkuu wa wilaya huyo amewasihi wahitimu kutumia maarifa walio yapata kama nyenzo ya kuwatumikia na kuwahudumia Wananchi na waumini kwa weledi na ufanisi zaidi.                     

Katika Mahafali hiyo wahitimu 15 wamefanikiwa kuhitimu na wamepata fursa ya kujifunza fani mbalimbali ikiwemo Uwakili wamuda, Fedha na Mazingira, Upatanisho na Msamaha, Uhusiano wa Kanisa na Jamii, Ndoa na Maridhiano, Theolojia ya Biblia na Tafiti mbalimbali katika Jamii.                           

Chuo cha Biblia ECLEA ni miongoni mwa vyuo muhimu vinavyo saidia kufundisha, Kulea na kuaandaa Wataalamu wa theolojia na viongozi wa dini na jamii.                          

Post a Comment

0 Comments