Mwana wa kiongozi mkuu wa Hezbollah auawa katika shambulio la Israel

 


Wanamgambo watano wa Hezbollah - wapiganaji wenye uwezo wanaoungwa mkono na Iran nchini Lebanon - wameuawa katika shambulio la Israel huko Beit Yahoun, kusini mwa Lebanon, kulingana na kundi la Kiislamu la Shia.


Abbas Raad, mwana wa kiongozi mkuu wa Hezbollah na mbunge wa Lebanon Mohammad Raad alikuwa mmoja wao, kundi hilo linasema.


Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, jumla ya wapiganaji 85 wa Hezbollah sasa wameuawa tangu ghasia kuzuka katika mpaka wa Israel na Lebanon.


Jeshi la Israel lilisema lilishambulia maeneo kadhaa ya Hezbollah nchini Lebanon siku ya Jumatano jioni, ikiwa ni pamoja na "miundombinu ya ugaidi" na "vikundi vya ugaidi" vilivyojaribu kurusha makombora ndani ya Israeli na kuwarushia wanajeshi wa Israeli.


Hezbollah ndio jeshi kubwa zaidi la kisiasa nchini Lebanon na llimeorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uingereza, Marekani na Umoja wa Kiarabu.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items