Afisa mkuu wa Israel asema hakuna mateka atakayeachiliwa kabla ya Ijumaa

 


Tzachi Hanegbi, mkuu wa Baraza la Usalama la Taifa la Israel, amesema mateka wa Israel hawataachiliwa na Hamas kabla ya Ijumaa.


"Mazungumzo ya kuachiliwa kwa mateka wetu yanaendelea," ameongeza katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.


Ilitangazwa jana usiku kuwa Israel na Hamas wamefikia makubaliano ya kubadilishana mateka 50 wanaoshikiliwa huko Gaza kwa mapumziko ya siku nne katika mapigano.


Makubaliano hayo pia yatashuhudia wanawake na watoto wa Kipalestina 150 wanaoshikiliwa katika jela za Israel wakiachiliwa huru na ongezeko la misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kuingia Gaza.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items