Rais Biden na Xi Jinping wa China kukutana kujadili ushindani na uimarishaji wa mawasiliano


White house ya Marekani imesema rais Joe Biden na rais wa China Xi Jinping watajadiliana kuhusu kuimarisha mawasiliano na kukabiliana na ushindani watakapokutana pembeni ya mkutano wa ushirikiano wa kiuchumi na mataifa ya Asia- APEC wiki hii.


Mkutano huo wa ana kwa ana utakaofanyika huko San fransisco Bay Jumatano utakuwa wa kwanza kati ya Biden na Xi kwa mwaka mmoja, wakati wanadiplomasia hao wa juu wanatarajia kuondoa mivutaano katika mataifa hayo yenye nguvu.


Mshauri wa maswala ya usalama wa White House Jake Sulivan aliwaambia waandishi wa habari kwamba Biden anaamini hakuna mbadala wa diplomasia ya ana kwa ana ili kudhibiti uhuaiano huo mgumu.


Sulivan amesema Biden atakwenda katika mkutano huo akiwa na msimamo imara, akiwa ameiweka Marekani mbele katika ushindani ndani na nje na katika kujikwamua kwa hali ya juu ya kupanda kwa gharama ya maisha katika uchumi wowote unaoongoza.


Amesema Washington inatarajia matokeo yoyote maalumu kutokana na Mkutano huo na kutegemea kupiga hatua kuimarisha majeshi na ushirika wa CHINA na kupambana na biashara ya dawa aina ya fentanyl ambayo imekuwa janga Marekani

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items