VIDEO: Rais Samia tunaomba tulipwe hela zetu, sisi hatuna mgogoro-wananchi Kipunguni


Wakazi 524 wa Mtaa wa Kipunguni kata ya Kipawa jiji la Dar es salaam wamemuomba Rais Samia kuingilia kati ili wajue hatma yao ya kulipwa au kutokulipwa eneo lililofanyiwa tathmini ya kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege.

Wakizungumza kwenye mkutano uliofanyika leo Novemba 15, 2023 wamemuomba Rais Samia kuwalipa fidia haraka kwani kwa sasa wamekua hawajui hatma yao.

''Tunamuomba Rais Samia aingilie kati tulipwe pesa zetu hiki ni kilio cha muda mrefu hatujui tunaishije maisha yetu yamekuwa magumu, Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba alikua atatuambia pochi la mama limetuna kwahiyo kama limetuna basi tulipeni ili tuondoke na hapa hakuna mgogoro wowote mkija kutulipa hata kesho tunaondoka'' wamesema wananchi

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items