Waasi wa Houthi wa Yemen wateka nyara meli ya shehena ya Israel katika Bahari Nyekundu

 


Waasi wa Houthi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran wanasema wamekamata meli ya mizigo ya Israel katika Bahari Nyekundu.


Walisema meli hiyo kisha ilipelekwa katika bandari ya Yemen.


Hata hivyo, Israel imesema meli hiyo haikuwa yake, na hakuna Waisraeli waliokuwa miongoni mwa wafanyakazi wake. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema hiki ni "kitendo kingine cha ugaidi wa Iran".


Iran haijatoa maoni yoyote. Waasi wa Houthi walikuwa wametishia kuteka nyara meli ya Israel iliyo karibu kutokana na vita vya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.


Israel inasema watu 1,200 waliuawa na zaidi ya 240 walichukuliwa mateka wakati wa shambulio la kushtukiza la Hamas kusini mwa nchi tarehe 7 Oktoba.


Israel imeanzisha operesheni kubwa ya kijeshi - inayohusisha mashambulizi ya anga na mizinga pamoja na wanajeshi wa nchi kavu - kwa lengo la kuwaondoa Hamas.


Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas inasema idadi ya waliofariki Gaza tangu wakati huo imefikia 12,300. Zaidi ya 2,000 wanahofiwa kuzikwa chini ya vifusi.


Waasi wa Houthi wamerusha makombora kadhaa na ndege zisizo na rubani kuelekea Israel mara tu baada ya Israel kuanzisha operesheni yake ya kulipiza kisasi.


Marekani ilisema wakati huo kwamba makombora yote na ndege zisizo na rubani yalinaswa na meli yake ya kivita katika Bahari Nyekundu.


Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilielezea shambulio la meli hiyo - ambalo halikutaja - kama "tukio baya sana la matokeo ya ulimwengu".


IDF ilisema meli hiyo ilikuwa ikitoka Uturuki kuelekea India ilipokamatwa kusini mwa Bahari Nyekundu karibu na Yemen.


Ingawa Israel inasema meli iliyokamatwa haina uhusiano wowote nayo, ripoti ambazo hazijathibitishwa zinaonyesha kuwa meli hiyo inaweza kuwa mmiliki wake ni raia wa Israel.


Katika taarifa ya Jumapili kwenye mtandao wa kijamii, Bw Netanyahu alisema kuwa Israel "inalaani vikali shambulio la Iran dhidi ya meli ya kimataifa".


Alisema meli hiyo inamilikiwa na "kampuni ya Uingereza na inaendeshwa na kampuni ya Kijapani", na kuongeza kuwa "wafanyakazi 25 wa mataifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ukraine, Bulgarian, Filipino na Mexico" walikuwa ndani ya meli hiyo.


Mapema mwezi huu, Wahouthi waliiangusha ndege ya kijeshi ya Marekani isiyo na rubani kwenye pwani ya Yemen, maafisa wa Marekani walisema.

Post a Comment

0 Comments