Wananchi wamshukuru Mbunge kupata daraja.

 


Na John Walter-Babati

Wananchi wa kitongoji cha Mpakani kata ya Qash,  wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini kwa kutimiza ahadi aliyoitoa kwao ya kuwajengea daraja ambalo lilikuwa kilio chao cha muda mrefu.

Wakizungumza mbele ya Mbunge huyo alipofika kijijini hapo kukagua miundombinu ya barabara katika kipindi hiki cha mvua, wakazi hao wamemueleza kuwa hivi sasa wanapita bila wasiwasi na kusafirisha mazao yao baada ya daraja hilo kukamilika.

“Tunakushukuru  sana mbunge wetu  kwa ujenzi wa daraja hili, kwani limekuwa mkombozi kwetu kwani hapo nyuma Wakinamama walikuwa wakijifungulia njiani kufuatia vyombo vya usafiri kushindwa kupita ila kwa sasa mambo yapo vizuri, asante sana" alisema Halima Rashid

Naye Mheshimiwa Sillo ameahidi kuendelea kuwatumikia wananchi hao kwa kutimiza ahadi mbalimbali alizotoa.

Aidha amewasihi wananchi hao kutunza daraja hilo ili liendelee kudumu kwani serikali inatumia gharama kubwa kujenga na kukarabati miundombinu ya barabara.

Post a Comment

0 Comments