Na John Walter-Manyara
Kampuni ya Mati Super Brands Ltd imewafariji waathiriwa wa Mafuriko na maporomoko ya Matope, mawe na miti yaliyotokea Desemba 3, wilayani Hanang' na kusababisha vifo, Majeruhi na wengine wakikosa makazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo David Mulokozi amemkabidhi Waziri wa nchi,ofisi ya Waziri mkuu sera, bunge na uratibu Jenista Mhagama misaada mbalimbali ikiwemo Vyakula kama mahindi yaliyokobokewa kilo 700, maharage guna 6 sawa na kilo 600, ,mchele Kilo 1000 ,chumvi katoni 10, Mafuta ya kupikia lita 200,sabuni za mche, taulo za kike,mafuta ya kupaka, pamoja na kuchangia shilingi milioni 10 kwenye mfuko wa Maafa.
Waziri Mhagama ameishukuru kampuni hiyo Kwa mchango waliutoa katika kipindi hiki kigumu.
Mpaka sasa Majeruhi katika Maafa wanatajwa kufikia 115 na miili iliyopatikana mpaka sasa na kutambuliwa na ndugu zao ni 65.
Mati Super Brands Ltd ni Kampuni ya kizalendo inayozalisha vinywaji changamshi vikiwemo Strong Dry Gin, Sed Pineapple Flavoured Gin, Strong Coffee na Tanzanite Premium Vodka huku makao makuu yake yakiwa Mjini Babati mkoani Manyara.
0 Comments