Na John Walter-Babati
Wanadamu wametakiwa kuendelea kumtumikia Mungu hata wakati wa magumu wanayopitia.
Hayo yameelezwa na Mwinjilisti Lazaro Stephano wakati wa ibada ya Jumapili iliyoenda sambamba na harambee ya chagizo kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kaskazini kati Jimbo la Babati, Usharika wa Magara Mtaa wa Moya.
Mwinjilisti amesema wakati wa Magumu baadhi ya watu wanamsahau Mungu na kwamba pindi Bwana yesu Kristo atakaporudi atawachukua wale wenye imani ya kweli.
Amesema mfano halisi wa maisha ya Binadamu mwenye Imani ya kweli ni pale panapotokea changamoto,wapo wanaotoa msaada na wengine hukimbia kabisa.
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo Daniel Sillo ametoa sadaka ya Shilingi laki Tano Kwa ajili ya kusaidia kwaya ya Mkombozi kununua vifaa vya muziki.
Sillo ametumia maandiko matakatifu kutoka kitabu cha Ezra 10-4 unaosema Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende.
0 Comments