Aliyemuua mkewe nae ajinyonga


Mwanamke mmoja aliefahami kwa jina la DOTO MAGAMBAZI mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa Mjimwema kata ya Kiluvya wilayani Kisarawe amefariki dunia baada ya kukatwa katwa na mapanga katika sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyopeleka kufariki dunia akipatiwa matibabu katika hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha Mkoani Pwani.

Kamanda wa jeshi la polis mkoa wa Pwani ACP - PIUS LUTUMO akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya Habari amesema mnamo mach 17 mwaka huu marehemu alivamiwa na kukatwa mapanga na majira ya 03:45 usiku na kufariki 05:00 wakati akipatiwa matibabu masaa machache baada ya kufikishwa hospitali.

Aidha kamanda LUTUMO ameendelea kusema katika uchunguzi wa awali jeshi lake limefanikiwa kubaini kuwa aliehusika na shambulio hilo ni aliekua mume wa marehemu aliefahamika kwa majina MBARAKA HARUNA MAPUNDA umri miaka 42 ambae ni mkazi wa Chanika Dar es salaam aleitalakiana nae mwaka mmoja uliopita sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi ikiwemo kugombea mali walizochoma na marehemu.

Hata hivyo wakati jeshi la polis mkoa wa Pwani wakati likiendelea na msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa huyo aliekua mume wa marehemu likamkuta amejinyonga.

Mtuhumiwa huyo alikutwa vichakani akiwa amejining’iniza kwenye mti kwa kutumia mkanda wa suruali ikiwa ni umbali wa mita mia tatu kutoka nyumbani hapo mtaa wa Mjimwema kata ya Kiluvya huku sababu ikitajwa kuwa ni kukwepa mkono wa jeshi la polis lililokua likimsaka kutokana na mauaji ya mtalaka wake.

Jeshi la polis limewataka watu kutojichukulia sheria mkononi, marehemu hao wawili wameacha watoto watatu yatima.

Post a Comment

0 Comments