Joto la uchaguzi CHADEMA lashika kasi,wanaoutaka uongozi wajitokeza kwa kasi kuchukua fomu









Njombe

Wanachama pamoja na baadhi ya waliokuwa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Njombe wameendelea kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama hicho.

Muamko mkubwa wa wanachama umeendeleo kuonekana ndani ya Chama hicho kuanzia ngazi ya kata,jimbo,wilaya na sasa ngazi ya mkoa huku watia nia wakieleza sababu za kutaka kuongoza chama hicho ambapo wengi wao wakidai kuwa nia yao ni kutaka kuendelea kuimarisha chama ili kiweze kuja kushika dola na kukitoa madarakani Chama cha Mapinduzi (CCM)

Baraka Kivambe ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Njombe amesema nafasi zilizotajwa na kugombewa ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA,uenyekiti baraza la wazee,uenyekiti wa baraza la wanawake pamoja na nafasi ya ukatibu wa baraza la wanawake.

"Mimi niwatakie kila laheri kwasababu uchukuaji na urejeshaji wa fomu ni hatua kuelekea kwenye uchaguzi"amesema Kivambe

Ahad Mtweve ni mgombea wa nafasi ya uenyekiti mkoa wa Njombe mara baada ya kuchukua fomu amesema lango lake kubwa ni kwenda kulinda heshima ya Chama kwa kuwapata viongozi wa kutosha watakaokwenda kuiongoza serikali katika chaguzi zijazo.

"Jambo la kwanza ni kulinda heshima ya Chama nitaka kuufanya mkoa wa Njombe kuwa ni mkoa ambao unafanya vizuri kwenya ngazi mbalimbali za serikali kwasababu tunatamani nafasi za ubunge kwenye majimbo yote ya mkoa wetu,madiwani lakini pia mwaka huu tunatamani kuchukua vitongoji na vijiji"amesema Mtweve

Ebron Mwakajungu ni mtia nia wa nafasi ya uenyekiti baraza la wazee amesema lengo kubwa kwake ni katika kupigania wazee kutokana na kazi kubwa waliyoifanya kulitumikia taifa huku Msifuni Mahenge ambaye ni mgombea wa nafasi ya ukatibu wa baraza la wanawake akidai kuwa lengo lake ni kwa ajili ya kuingia kwenye utendaji ili kuimarisha Chama hicho kwani awali amtumikia vya kutosha nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA wilayani Makete.

Post a Comment

0 Comments