Kamati ya bunge yampongeza rais Samia kufufua chuo cha Rwenzari Tabora.



Na. Mwandishi wetu - TABORA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufufua Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu Rwenzari ambacho kilikuwa hakifanyi kazi  takribani miaka 20.

Akizungumza Machi 13, 2024 Mkoani Tabora Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq amesema dhamira ya Mhe. Rais Samia ni kuhakikisha makundi ya watu wenye ulemavu wanapata fursa sawa za kushiriki katika kujenga taifa lao na kuishi katika mazingira salama.


Aidha, amesema mafunzo wanayopata wanafunzi Chuoni hapo yatawasaidia kujiajiri na kuanzisha mafunzo kwa watu wengine ili kuinua uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema miongono mwa maboresho yaliyofanyika ni pamoja na ununuzi wa samani, upanuzi wa kuta na vifaa kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia.


Naye, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ndg. Saidi Mabie, amesema serikali ilitotoa shilingi Mil. 689 kwa ajili ya kukarabati chuo hicho ambacho kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 129 katika kozi za uselemara, ubunifu ushonaji, kilimo bustani, uchomereaji na umeme wa majumbani.


Akitoa neno la shukrani Mwanafunzi wa Chuo hicho Amosi Yokram amemshuru Mhe. Rais kwa kuendelea kuwajali Watu Wenye Ulemavu na kuboresha miundombinu kwa ajili ya kupata elimu.

Post a Comment

0 Comments