Maelekezo ya LAAC baada ya kukagua jengo la utawala Babati DC.



Na John Walter-Babati
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imemaliza ziara yake ya siku tatu  katika mkoa wa Manyara kwa kutembelea jengo la utawala la halmashauri ya wilaya ya Babati na nyumba ya mkurugenzi ambayo ipo katika hatua ya ujenzi.

Baada ya kukagua majengo hayo LAAC imetoa mapendekezo yafuatayo.

Mkurugenzi ahakikishe fedha zilizobaki kiasi cha  shilingi Milioni 103 zinatumika kukamilisha mradi kufikia tarehe 10 mei,2024 kama ilivyoanishwa katika mkataba na sio kuomba fedha za nyongeza ofizi ya Rais TAMISEMI. 

Aidha ofisi ya Katibu tawala (RAS) mkoa wa Manyara  ifanye tathmini ya kina juu ya matumizi yaliyofanyika katika mradi huo na kuiwasilisha taarifa hiyo ofisi ya Rais TAMISEMI kabla ya April 30 mwaka huu.

Mkurugenzi ahakikishe samani za shilingi milioni 300 ambazo pesa zake zimeshapokelewa, zinanunuliwa kabla ya kukamilika kwa mwaka huu wa fedha.

Aidha CAG afanye uhakiki katika ukaguzi utakaofuata.

Mkurugenzi ahakikishe dosari zote zilizobainishwa na CAG katika mradi huu zinarekebishwa na CAG afanye uhakiki katika ukaguzi ujao.

Mkurugenzi ahakikishe utendaji wa kazi hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo unazingatia miongozo inayotolewa na ofisi ya Rais TAMISEMI.
 
Mkurugenzi aandae taarifa ya kina kuhusu matumizi ya shilingi Milioni 83 zilizopangwa kutumika kwa ajili ya uchimbaji wa kisima na  manunuzi ya AC na kuiwasilisha kwa CAG kabla ya machi 30.

Kwa Mujibu Mkurugenzi wa Babati vijijini Anna Mbogo, wamepokea shilingi bilioni 3.4 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala.

Ujenzi wa jengo hilo ulianza 30.4.2021 chini ya mkandarasi SUMA JKT na kwa sasa lipo katika hatua ya ukamilishaji.

Hata hivyo Halmashauri inaomba nyongeza ya shilingi Milioni 196 kutoka TAMISEMI kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la utawala kwa asilimia mia moja.

Post a Comment

0 Comments