Mapendekezo na maelekezo ya LAAC nyumba ya Mkurugenzi Babati.


Na John Walter-Babati

Mkurugenzi mtendaji amesema April 27,2022 walipokea shilingi Milioni 150 kutoka serikali kuu kwa ajili ya Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi mtendaji  katika mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo mradi huo ulianza agosti 2022.

Hadi sasa mradi umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 130 na imefikia hatua ya ukamilishaji sawa na asilimia 80 ya utekekezaji.

Mbogo amesema mradi huo unahitaji nyongeza ya shilingi Milioni 208 kwa ajili ya kujenga uzio, kibanda cha Mlinzi pamoja na kujenga nyumba ya mhudumu.

Baada ya taarifa hiyo kuwasilishwa mbele ya kamati ya LAAC ikiongozwa na makamu mwenyekiti Ester Bulaya, ikatoa mapendekezo na maelekezo yafuatayo;

Kwa kuwa stoo kuna vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 19.3 pamoja ba bakaa ya shilingi milioni 19.4 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi, mkurugenzi ahakikishe ujenzi wa nyumba hiyo unakamilika kabla ya kukamilika kwa mwaka huu wa fedha na dosari zote zilizoainishwa na CAG ziondolewe na taarifa iwasilishwe kwa CAG kwa ajili ya uhakiki.

Kabla ya machi 22, 2024 mkurugenzi awasilishe taarifa ya kina kwa CAG kuhusu kiasi cha fedha kilichotumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi ikiainisha kila hatua iliyofanyika katika ujenzi huo kwa mujibu wa BOQ pamoja na kubainisha sababu za kitaalamu zilizosababisha mradi huo kutokamilika kwa wakati tangu kuanza kwa utekelezaji wake agosti 16,2022.

Ofisi ya Rais TAMISEMI ifanye uchunguzi wa gharama halisi zilizotumika kutekeleza mradi wa nyumba ya mkurugenzi ili kubaini iwapo kuna thamani  ya fedha na iwapo  matumizi yamefanyika kama ilivyotarajiwa. 

Aidha kabla ya kuidhinisha kiasi chochote cha fedha za nyongeza kwa ajili ya kumalizia nyumba hiyo, ofisi ya rais TAMISEMI ijiridhishe juu ya uhalali wa maombi hayo.

Mkurugenzi ahakikishe vifaa vya mradi vilivyoharibika yaani simenti iliyoganda kutokana na uzembe wa kutotekeleza mradi kwa wakati vinafidiwa na waliosababisha uzembe huo na taarifa iwasilishwe kwa CAG kwa ajili ya uhakiki.

Kaimu mwenyekiti Ester Bulaya amewataka watendaji wa serikali kuisaidia serikali kusimamia miradi kwa uaminifu ili adhma ya kuwaletea wananchi Maendeleo itimie.

Post a Comment

0 Comments