Orxy kubadili maisha ya wafanyabiashara soko la Feri Dar, yaahidi kufunga mtambo wa nishati safi ya kupikia


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Gesi ya Oryx Tanzania, imewaahidi Mama na Baba lishe katika Soko la Samaki la Kimataifa Feri kuwafungia mtambo wa nishati safi ya kupikia ili kuwaepusha kutumia fedha nyingi kununua gesi kupitia mitungi midogo.

imesema hatua hiyo ni utekelezaji wa mkakati wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kulinda mazingira na kuwaweka wanawake na watoto katika nafasi nzuri ya kujiendeleza kiuchumi na kielimu.

Hayo yalielezwa jana na Mbunge wa Ilala ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge Hassan Zungu katika hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 200 iliyotolewa na kampuni hiyo kwa mama na baba lishe wa sokoni hap oleo Machi 22, 2024.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbasi Mtemvu, Mkuu wa Wilaya Ilala Edward Mpogolo na Mwenyekiti wa CCM wilayani humo Said Side.

Zungu alisema kuwa mitungi hiyo 200 ni sehemu ya mitungi 700 iliyotolewa kwa Mama na Baba lishe katika jimbo hilo ambayo imetolewa kwa ushirikiano wa Zungu na kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania.

Naibu Spika Zungu, ametoa Oryx imetoa ahadi hiyo baada ya kupokea maombi ya wafanyabiashara hao kupitia kwa kiongozi wa wafanyabiashara wa Zone Namba 7 katika soko hilo, Said Mpinji aliyelalamika kuwa wanalazimika kutumia sh. 110,000 kila siku kujaza gesi katika mitungi inayotumika kuendeshea shughuli zao.

Akijibu kilio hicho, Zungu alisema ni ya muda mrefu na kwamba tayari amezungumza na kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake, Benoit Araman ambaye amekubali kufunga mifumo ya gesi ya kisasa kisha kusambaza huduma hiyo kwa wafanyabiashara hao kwa gharama nafuu.

“Mkombozi wetu ni Rais DkSamia Suluhu Hassan ambaye alianzisha kampeni ya Nishati safi ya kupikia, kuhakikisha Watanzania wanaishi maisha mazuri.

“Oryx wamekubali kuweka mtungi mmoja mkubwa na mifumo ya usambazaji, kisha watasambaza huduma kwa mama na baba lishe waliopo hapa na kuwafungia mita ambazo watzitumia kulipia huduma kama wanavyofanya katika umeme,” alisema.

Kwa upande wake Benoit alisema Oryx wamewafikia wajasiriamali hao kwa lengo la kutekeleza mkakati wa Rais Dk. Samia wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kulinda mazingira na afya za wananchi.

Alisema kuwa tangu Julai mwaka 2021, Oryx walianza mkakati huo baada ya Rais Samia kutangaza kwamba serikali yake inataka kuona hadi mwaka 2030 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

“Kupika kwa kutumia gesi ya Oryx kuna faida nyingi ikiwemo kuwaepusha wanawake kutumia muda mwingi kutafuta kuni, kunawaepusha watoto kwenda umbali mradi na kutumia muda wao mwingi kutafuta kuni, aida kuwasaidia kupata muda mwingi wa kujisomea,” amesema.

Mwenykiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abbasi Mtemvu aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, amesema kilichofanyika ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kumpongeza Zungu kwa namna anavyowatetea wananchi katika jimbo lake.

“Zungu ni mfano wa kuigwa, amefanya makubwa. Nilikuwa naye bungeni kwa miaka 10 muda wote ameonyesha dhamira ya kutetea wananchi wa jimbo lake, anastahili pongezi,” almeeleza.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mgolo, amesema maelekezo yaliyotolewa na Naibu Spika Zungu kutaka ifanyike tathmini haraka kufanikisha Oryx kufunga mtambo huo atayatekeleza kwa haraka kwa kushirikiana na wenzake.

Hata hivyo, aliiomba Oryx kuangalia uwezekano wa mtambo kama huo kufungwa pia katika eneo la Zone Namba 4 ambako baba na mama lishe nao wanahitaji huduma hiyo.

Post a Comment

0 Comments