Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), George Katabazi na timu yake, Machi 12, 2024, amefanya ziara ya kutembelea na kukagua utendaji kazi wa vikundi vya ulinzi mtaa wa Maisaka Wilaya ya Babati Mkoani hapa
Ambapo, amekabidhi hati ya cheti cha Pongezi kwa viongozi wa Kikundi cha Ulinzi Mtaa wa Maisaka 'B' Halmashauri ya Mji Babati, Mkoani Manyara kwa kuonesha ushirikiano na kufanya kazi kwa uaminifu na weledi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi huku wakiishi kwa vitendo dhana na falsafa ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi mtaani
Akizungumza wakati akikabidhi cheti, SACP Katabazi, amewataka vikundi vya ulinzi kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria bila ya kumuonea wala kumpendelea mtu ili kuepuka malalamiko katika jamii
Amesema Jeshi la Polisi linahubiri dhana na falsafa ya Polisi jamii na ulinzi shirikishi Kila Leo ili kuimarisha vikundi vya ulinzi kuanzia ngazi ya kitongoji, Kijij, mtaa na kata.
Katika ziara yake Katabazi amefanya harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya mahitaji muhimu ya kikundi hicho ikiwemo filimbi, tochi na Makoti ambapo amewaomba na wadau wengine kujitokeza kusaidia vikundi vya kulinzi
Sambamba naye, mmoja wa Viongozi wa Kikundi hicho amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kutambua na kuthamini mchago wao na kutoa ahadi kuuendeleza na kuwaelimisha vijana wengine kujiunga katika vikundi vya ulinzi ili kushirikiana na Polisi katika kutokomeza uhalifu katika jamii
" kwa niaba ya Kikundi nashukuru Jeshi la Polisi kutupa cheti cha Pongezi, tutajituma zaidi ili tupatiwe zawadi kubwa zaidi" amesema kiongozi Kikundi Maisaka 'B'
Naye Mkuu wa Kamisheni ya Polisi Jamii Manyara Kamishna Msaidizi (ACP) Kija Mkoyi, amewataka vijana hususani bodaboda kuunda vikundi vya ulinzi katika maeneo yao ili kuimarisha ulinzi na usalma wao na Mali zao
0 Comments