TAEC yakagua matumizi ya mionzi nchini ''Mtu yeyote haruhusiwi kusafirisha chanzo cha mionzi'


Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) inaendelea na zoezi la ukaguzi wa matumizi  ya mionzi nchini kwa lengo la kujiridhisha kama matumizi ni salama katika maeneo ya hospitalini, viwandani, vituo vya utafiti, migodini, bandarini, viwanja vya ndege pamoja na katika ujenzi wa barabara na reli.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania TAEC Dkt. JUSTIN NGAILE baada ya kufanya ukaguzi katika hospitali ya wilaya ya Chato na Hospitali ya Rufaa ya Chato ambapo amesisitiza matumizi ya mionzi nchini ni lazima ya simamiwe vizuri ili kuwalinda wananchi, wafanyakazi na mazingira.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Post a Comment

0 Comments