Wajenga bweni kuimalisha miundo mbinu ya ujifunzaji kwa watoto wenye uhitaji maalum


Na Baraka Messa, Songwe.

PROGRAM jumuishi ya taifa ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto  katika sekta ya elimu inahimiza mazingira rafiki na shawishi kwa watoto wenye mahitaji Maalum  kuanzia miaka 0 mpaka miaka nane ili kumuwezesha kufurahia mazingira ya shule na kuuwezesha ubongo wake kukua kwa wakati kulingana na umri kama walivyo watoto wengine.


Katika Wilaya ya Ileje mkoani Songwe kumekuwa na changamoto ya Malezi na Makuzi kwa watoto wenye ulemavu hasa kunyimwa haki yao ya Msingi ya kupata elimu kuanzia elimu ya awali na Msingi kwa kisingizio cha ulemavu .

kutokana na changamoto za watoto wenye mahitaji Maalum kutopewa kipaumbele katika suala muhimu la elimu, Wilaya ya Ileje imeanza kuimalisha miundo mbinu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa bweni litakalo kuwa na uwezo wa kuchukua watoto wenye uhitaji Maalum 300 katika shule ya Msingi Ipapa.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Farida Mgomi amesema kumekuwa na changamoto nyingi kwa watoto wenye uhitaji Maalum ikiwa ni pamoja na kunyimwa haki yao muhimu ya kupelekwa shule.

Anasema jambo hilo limewasukuma Wilaya hiyo kuanzisha ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya msingi Ipapa iliyopo Kata ya Isongole Wilaya hapo ambapo  mpaka kukamilika litagharimu Sh 100 milioni.

"Kukamilika kwa bweni hilo kutatua changamoto za watoto wengi wenye mahitaji maalum kuanzia elimu ya awali na Msingi kupata haki yao ya Msingi ya kupata elimu, hasa wale wanaofichwa majumbani" amesema

Mgomi amemwagiza mkandaras anayesimamia bweni hilo kulikamilisha haraka ili kupunguza adhaa kwa wanafunzi 300 wenye ulemavu kupata elimu bora.

Agizo  hilo  amelitoa  leo Machi 22,2024  na kwamba  amesikitishwa na kusasua kwa ujenzi wa  bweni hilo  licha ya kuwepo kwa vifaa kama  rangi,saruji hali imebainika  ni usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo.

Amesema awali serikali ilitoa fedha Sh, 100 millioni kwa ajili ya kukamilisha mradi huo ili kupunguza adha kwa wanafunzi 300 wenye ulemavu kupata elimu bora na kuondoa changamoto zinazowakabili.

Amesema  Serikali baada ya kuleta milioni 100 za awali imeongeza tena Sh ilingi milioni, 158 kwa ajili ya  ujenzi wa  bweni na uzio niwatake  simamieni hizi fedha hatutawavumilia zitatumika tofauti na maelekezo.
 
Kwa upande wake Mwita Isaya kutoka Asas isiyo ya kiserikali ya HIMSO ambayo ni kinara katika masuala ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali katika mkoa wa Songwe amesema Wilaya ya Ileje na mkoa wa Songwe kwa ujumla kumekuwa na changamoto ya Malezi yanayopeleke mtoto kutofikia ukuaji sahihi.

" Katika mkoa wetu wa Songwe kati ya watoto 100 ni watoto 24 ndio wanapitia malezi sahihi yenye mwitikio, wazazi na Jamii ya mkoa wa Songwe inatakiwa kubadilika katika masuala muhimu ya kulea watoto na kuhakikisha wanapata elimu muhimu kuanzia elimu ya awali " amesema Chacha.

Akiongelea kuhusu wa wazazi ambao wamekuwa na tabia ya kuwaficha watoto walemavu amewataka kuacha na badala yake wawape nafas ya kupelekwa shule kupata elimu kuanzia elimu ya awali ili wawe na uwezo wa kujitegemea kwa baadae.

Mwananchi Samsoni Mshani amesema kukamilika kwa bweni hilo la watoto wenye mahitaji Maalum kutasaidia na  kuhamasisha wananchi wengi kupeleka watoto walemavu kupata masomo, kwa sababu wengine huogopa kuwapeleka shule kwa sababu ya watoto wengi kuhitaji ukaribu wa kuwasindikiza kila siku , jambo ambalo huona kama shughuli zao husimama.

" Kukiwa na bweni wengi wataleta watoto kwa sababu , wazazi au walezi hawatapata usumbufu wa kuwapeleka na kuwafuata watoto asubuhi na muda wa kurud shule" amesema Mshani.

Mwongozo wa Serikali wa mwaka 2016 wa elimu bila malipo hujumuisha elimu ya awali kwa watoto wote waliofikia umri wa sahihi kuanza masomo bila kubagua walemavu.

Post a Comment

0 Comments