Wananchi watakiwa kufuata miongozo ya utunzaji Mazingira


Na John Walter -Babati

Wananchi wa wilayani Babati, wametakiwa kuhakikisha wanatunza na kuhifadhi mazingira ili yawe endelevu kwa vizazi vijavyo.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wilaya ya Babati, Halfan Matipula katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Boay kikiwahusisha Wakala wa Misitu Tanzania wilaya ya Babati.

Matipula alisema katika kijiji hicho lipo tatizo la uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu ambazo ni pamoja na uchomaji misitu, ukataji wa miti na uharibifu wa vyanzo vya maji.

Pia alizitaja athari zinazotokana na shughuli hizi za kibinadamu kuwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi, kupungua na kunyesha kwa mvua bila mpangilio na kusababisha mafuriko, kutokea kwa ukame.

Amewataka wananchi kufuata sheria na miongozo ya uhifadhi wa misitu na mazingira kwa ujumla ili kuepusha madhara yatokanayo na uharibifu huo kama inavyoshudiwa maeneo mbalimbali Nchini.

"Kama misitu haitalindwa na kuacha wananchi kutumia wanavyotaka basi haitokuwepo" alisema Matipula

Aidha amewataka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wilaya ya Babati kutoa elimu kwa wananchi mara Kwa mara juu ya umuhimu wa kuilinda misitu.

Post a Comment

0 Comments