FCC Yaandaa Iftar kwa wafanyakazi na wadau wake


TUME ya Ushinda Tanzania (FCC) imeandaa Iftari kwa wafanyakazi pamoja na wadau wa tume hiyo, hafla iliyofanyika katika hoteli ya Rotana, jijini Dar es Salaam jana Aprili 9, 2024.

Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Sheikh Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, ambaye aliwakilishwa na Abdallah Salum akiwakilisha waumini wa dini ya Kiislam ambao wapo kwenye mfungo wa mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.


Akizungumza katika hafla hiyo, mwakilishi wa Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Abdallah Salum amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw. William Erio kwa kuandaa Iftari hiyo kwa wafanyakazi pamoja na wadau huku akiwaomba wafanyabiasha na waumini wa dini ya Kiislam kuwa na hofu mungu kwa kuendeleza kutenda mambo mema yaliyoamrishwa kwenye vitabu kwa kipindi chote cha maisha.

''Tupo kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhani na hapa nitumie fursa hii kuwaomba Wafanyabiashara hapa leo tumekutana kwa sababu ya Tume ya Ushindani na ushindani upo kwenye biashara, mnapofanya biashara zenu msiangalie faida zaidi, waangalieni na watu wa hali ya chini, nchi inawahitaji sana lakini lazima muwe na hofu ya mungu ili muendelee kupata baraka kwenye biashara zenu'' amesema Sheikh Abdallah Salum


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw, William Erio amewapongeza wafanyakazi na wadau wote kwa kuhudhuria hafla hiyo ambayo imewakutanisha kwa pamoja kupata futari na mawaidha ya kumcha mungu kwenye mwezi huu mtukufu na hata kwenye maisha ya kila siku hususani kwenye majukumu ya kazi.

''Hapa leo sisi kama wafanyakazi na wadau tumepata ujumbe mzuri na tuondoke nao kwenda kuufanyia kazi na tunapotekeleza majukumu yetu kama wanadamu tunahitaji kumcha mungu kwa wakati huu na ikipendeza hadi ramadhani nyingine na tumefanya haya kwa kuzingia yale tuliyotakiwa kuyafanya na ujumbe huu unahusu nyendo zetu wote '' amesema Bw, Erio. 

 

Wakurugenzi wa Tume ya Ushinda (FCC) waliohudhuria kwenye Iftari iliyoandaliwa na Tume hiyo jana Aprili 8, 2024 kwenye hoteli ya Rotana jiji Dar es salaama. Kutoka kushoto ni Zaytun Kikula Mkurugenzi wa Utafiti, Muunganisho na Utetezi, Khadija Ngasongwa Mkurugenzi wa udhibiti wa bidhaa Bandia na Magdalena Utouh Mkurugenzi wa Udhibiti wa Mienendo ya Biashara
Post a Comment

0 Comments